Hatimaye Mahakama Yakubali Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo Apewe Dhamana




hughulikia dhamana ya mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili. Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini.

Shtaka la pili ni kutoa taarifa za uongo kwa watumishi wa umma mjini Mafinga alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha Polisi Mafinga kuwa alitekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto cha Mafinga.

Alifikishwa  mahakamani hapo saa tatu asubuhi akiwa kwenye gari la Polisi kisha kupelekwa katika mahabusu ndogo mahakamani hapo na kuingizwa katika chumba cha mahakama saa 3:45 asubuhi. Kesi imeahirishwa hadi Aprili 4, 2018.

Mara ya kwanza Nondo alipofikishwa mahakamani kuliibuka mkanganyiko kwa kisheria kuhusu dhamana baada ya upande wa mashtaka kuomba asipewe kwa maelezo kuwa bado maisha yake yapo hatarini.

Comments

Popular posts from this blog

FACTORS THAT DETERMINE THE CONTENT OF TOPOGRAPHICAL MAPS.

MAP READING AND INTERPRETATION

CARTOGRAPHY AND MAP PROJECTION